Mahakama kuu Nairobi, Kenya imeamua kuliondoa jina la Rais Uhuru Kenyatta kwenye kesi kwa ikidai kuwa mashtaka ya uhalifu au madai hayawezi kufunguliwa dhidi ya Rais kwa kusema rais ana kinga ya kutoshtakiwa.

Kutokana na msingi huo wa kisheria, Jaji Chacha Mwita ameliondoa jina la Rais huyo kwenye kesi inayomkabili iliyofunguliwa na mwanaharakati Okiya Omtatah akipinga uamuzi wake wa kuteua makatibu wakuu na makatibu tawala.

Ingawa Jaji Mwita hakutoa sababu za kuliondoa jina la Rais Kenyatta kwenye kesi hiyo, kwa namna fulani ni kama alikubaliana na maoni ya Mwanasheria Mkuu kwamba Rais ana kinga ya kutoshtakiwa.

”Kwa maoni yangu, jina la Rais halipaswi kuweno katika ombi hili. Nitaeleza sababu katika hukumu ya mwisho ,” amesema Jaji Mwita.

Mwanasheria mkuu kupitia mwanasheria mwandamizi Jennifer Gitiri ameomba mashtaka hayo yafutwe na kuondolewa kwa jina la Rais Kenyatta katika suala linalojadiliwa kwamba ni kinyume cha katiba kuanzisha mashtaka yoyote dhidi ya Mkuu wa Serikali.

Tunasisitiza kwamba rais hawezi kushtakiwa kwani anafurahia kinga ya rais” ameongezea Gutiri

Katika kesi hiyo, Omtatah aliwashtaki Rais Kenyatta, Tume ya Utumishi wa Umma, Mwanasheria Mkuu na Spika wa Bunge juu ya uteuzi wa Baraza la Mawaziri.

Uganda hatarini kukatiwa misaada na UNHCR
400 wakabidhiwa kadi za CCM