Nchini Kenya, Daktari mstaafu Dkt. Moses Njue ameshtakiwa Mahakama ya Meru kwa kosa la kuiba viungo vya maiti za binadamu wakati wa utumishi wake.

Mwendesha mashtaka wa kesi hiyo, Claire Murithi ameiambia Mahakama kuwa Dkt. Njue aliiba moyo wa polisi wa zamani wa nchi hiyo, Benedict Karau huku akimtuhumu pia kupoteza ushahidi wa kesi hiyo.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa mahakamani Machi 12, 2015 Dkt Njue ambaye ndiye aliekuwa kiongozi mkuu wa uchunguzi wa maiti kiatika hospitali ya Consolata aliiba moyo kwa ajili ya kufundishia wanafunzi.

Hata hivyo Dkt. Njue amekana mashataka hayo yanayomkabili huku mahakama ikimtaka kuweka dhamana ya zaidi ya shilingi milioni 45 za kitanzania.

Aidha wakili wa Dkt. Njue ameiomba mahakama kupunguza dhamana hiyo kwa kile alichokidai kuwa mteja wake ni mtumishi wa umma ambaoi baadae Makajakama ilimtaka kutoa zaidi ya milioni 11 za kitanzania kama dhamana.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Kigwangalla ashangazwa na watanzania wanaosubiri kuajiliwa, 'Maisha hayakusubiri'
Vichanga Mapacha wafa kwa kuchomwa hospitalini