Mwanaume mmoja wa Florida anakabiliwa na kifungo cha miaka 11 jela baada ya kumuua mwanamke kwa kumpiga ngumi moja usoni katika bar iliyoko Daytona Beach.

Kwa mujibu wa Jarida la Daytona Beach News, Mahakama ya Florida imeamuru kuwa baada ya kutumikia kifungo hicho, Michael Lamothe mwenye umri wa miaka 36 atawekwa chini ya kipindi cha uangalizi kwa miaka nane.

Lamothe ameshtakiwa kwa kosa la kumuua Debra Jost mwenye umri wa miaka 54 katika mtafaruku uliozuka katika bar iitwayo Oyster.

Kwa mujibu wa ripoti ya uchunguzi wa polisi, Lemothe alikuwa amekaa nyuma ya mwanamke huyo na baadaye kumfuata na kumkumbatia kwa nyuma.

Kisha, Lamothe anadaiwa kumshika matiti na ndipo mwanamke huyo alipomsukuma na kumjia juu, ulizuka mvutano kabla mwanaume huyo hajaachia kombora la ngumi lililosababisha kifo cha mwanamke huyo.

Majaliwa awatoa hofu wakulima wa Pamba
Dkt. Abbas afunguka kuhusu mamilioni ya JPM

Comments

comments