Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha jana ilitoa uamuzi wake na kumpa dhamana mbunge wa Arusha Mjini, Godless Lema.

Lema alikuwa rumande akisubiri uamuzi wa Mahakama hiyo kufuatia kesi ya uchochezi dhidi yake, dhamana iliyozuiwa kwa maombi ya mawakili wa upande wa Serikali uliowasilisha hati ya kiapo ya Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Arusha (RCO).

Baada ya kupitia hoja za upande wa Serikali, Hakimu Kamugisha wa mahakama hiyo alisema, “nimeshindwa kupata kifungu chochote cha sheria ambacho kinazuia kutoa dhamana kwa mtuhumiwa aliye nje kwa dhamana ambaye ametenda makosa mengine ambayo hayahusiani na masharti ya dhamana ya awali.”

Baada ya kujiridhisha kwa uchambuzi wa kisheria, Hakimu aliamua kutoa dhamana kwa Lema.

Hata hivyo, Mawalikili wa Serikali walikata rufaa Mahakama Kuu kupinga uamuzi wa kumpa dhamana mbunge huyo, hali iliyopelekea kurudishwa rumande akisubiri hatima ya uamuzi wa rufaa hiyo katika Mahakama Kuu.

Kutokana na uamuzi huo, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu alisema kuwa chama hicho kimewataka mawakili wake, Tundu Lissu na Peter Kibatala kwenda jijini Arusha ili waongeze nguvu kwa mawakili waliokuwa wakiongozwa na John Mallya

Chukua Hii: Wataalam watoa toleo la TV inayofukuza Mbu
Video: Zitto agusa hisia za wabunge akiaga mwili wa Sitta