Mahakama nchini Afrika Kusini imemhukumu kifungo cha maisha jela mwanaume mwenye umri wa miaka 23 baada ya kumkuta na hatia ya kuwaua kwa kutumia shoka wazazi wake wote wawili pamoja na kaka yake.

Henri Van Breda, aliongezewa kifungo kingine cha miaka 15 kwa kosa la kujaribu kumuua mdogo wake wa kike, Marli, alipofanya shambulizi hilo Januari 2015.

Jaji Siraj Desai wa Mahakama Kuu, akisoma hukumu hiyo alisema kuwa Breda alifanya mauaji ya kikatili na shambulizi la kijambazi dhidi ya familia yake.

Mmoja kati ya mashahidi wa kesi hiyo ambaye ni mfanyakazi wa kitengo cha dharura, alisema kuwa tukio hilo lilikuwa baya zaidi kuwahi kushudia katika miongo minne aliyofanya kazi hiyo.

Henri Van Breda

Akiwa na umri wa miaka 20 wakati huo, Van Breda alitumia shoka kumchinja mama yake mzazi, Teresa akiwa na umri wa miaka 55, baba yake Martin mwenye miaka 54 na kaka yake Rudi aliyekuwa na umri wa miaka 22.

Alifanya mauaji hayo wakati ambapo familia hiyo ilikuwa imelala.

Van Breda alikana kufanya kitendo hicho akidai kuwa yeye pia alikuwa mhanga wa tukio hilo kwani kuna mtu mwingine aliyevunja nyumba na kuishambulia familia hiyo kwa shoka.

Mwanasheria wake amedai kuwa watakata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

Video: Mgalu afunguka kuhusu vituo vya Umeme
Foleni ya Tazara mwisho Septemba

Comments

comments