Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, imemkuta na hatia Mwanamuziki Judith ‘Lady Jay Dee’ Wambura kwa kuwatolea maneno ya kashfa, mmiliki wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Ruge Mutahaba.

Jay Dee amekutwa na hatia katika kesi hiyo iliyofunguliwa Mei 2013 na uongozi wa kampuni hiyo ambao walimlalamikia kwa kuwatolea maneno yenye kashfa kwenye mitandao ya kijamii.

Mahakama hiyo imemuamuru Mwanamuziki huyo kuwaomba radhi walalamikaji kupitia chombo cha habari chenye wigo mpana zaidi nchini au hata duniani.

Saa chache kabla ya Mahakama hiyo kutoa hukumu, Lady Jay Dee alipost picha kwenye Instagram na kuandika, “I am not afraid God is with me all the time (sina woga, Mungu yuko nami wakati wote).”

Jay Dee aka Binti Komando amekuwa katika mtafaruku mkubwa na Clouds Media Group kwa muda mrefu. Mwaka 2013, Ruge alizungumza kupitia Clouds Fm na kutoa uamuzi hewani kuwa wimbo wa Jay Dee aliomshirikisha Profesa Jay ‘Joto Hasira’ na nyingine zisichezwe tena.

lady-jay-dee

Jay Dee alikuzwa na uongozi wa Clouds Media Group wakati anaanza muziki, kabla ya kubadilika na kuwa hasimu wao akidai kuwa ni wanyonyaji. Aliyekuwa mumewe, Gardner G. Habash aliachana na kituo hicho na kuanza kusimamia kazi za muziki za Jide.

Hata hivyo, baada ya wana ndoa hao kuachana, alirejea tena na kuendelea kutangaza katika kituo hicho akipewa mkataba mnono.

Endt Awasemea Mbovu Inter Milan, Adai De Boer Alipaswa Kubaki
Serikali yamjibu Mbowe, 'hatufanyi kazi kwa miujiza'