Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imemuachia kwa dhamana Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu  baada ya kuwekwa mahabausu kwa siku kadhaa.

Tundu Lissu ambaye pia ni Rais Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) amepewa dhamana hiyo baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili wenye bondi ya shilingi Milioni 10 kila mmoja na kuzuiwa asitoke nje ya Dar es Salaam na kesi imeahirishwa hadi August 24 mwaka huu.

Awali, Tundu Lissu alikamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Dar es Salaam na kushikiriwa na jeshi la Polisi ambapo alikfikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka ya uchochezi.

Lissu alisomewa mashtaka ya kutoa lugha ya uchochezi dhidi ya Serikali, ambapo Mawakili wa upande wa Jamhuri waliiambia Mahakama kuwa Lissu alitenda kosa hilo la Julai 17, 2017 katika eneo la Ufipa, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Lissu apata dhamana, hatma ya upelelezi wa kesi yake yaanikwa
Muasisi wa jina ‘Bongo Flava’ aanzisha kipindi cha historia ya Muziki huo