Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo imemuchia huru mfanyabishara ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya VIP Engineering, James Rugemalira aliyekuwa anakabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi.

Hatua hiyo ya Mahakama imekuja baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuieleza mahakama hiyo kuwa hana nia ya kuendelea na shauri dhidi ya mfanyabiashara huyo.

Mwanasheria wa Rugemarila, Mike Ngalo amewaambia waandishi wa habari kuwa mteja wake yuko huru kwakuwa DPP amewasilisha nia ya kutoendelea na kesi dhidi yake.  

Rugemarila na mwenzake, Harbinder Sethi ambaye ni mmiliki wa Kampuni ya kufua umeme ya IPTL, walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Juni 19, 2017 wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 27/2027 yenye mashtaka 12, wakituhumiwa kujipatia fedha  kwa njia isiyo halali katika akaunti ya Tegeta Escrow.

Awali, wawili hao pamoja na aliyekuwa Katibu wa IPTL, Joseph Makandege walishtakiwa kwa makosa sita ya kughushi, kuwasilisha nyaraka za uwongo, kujipatia fedha kwa udanganyifu, uhujumu uchumi na kuisababishia Serikali hasara ya Sh358 bilioni.

Juni 16, 2021, Mahakama ilimkuta Seth na hatia ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, ambapo alilipa fidia ya Sh 26 bilioni na kuachiwa huru.

Kesi dhidi ya Seth na Regamalira inatokana na Sakata la Escrow lililoibuliwa bungeni mwaka 2014, ambapo ilielezwa kuwa fedha zilizokuwa zimewekwa kwenye akaunti maalum ya ‘Escrow’ iliyofunguliwa katika Benki Kuu ya Tanzania, ikisubiri uamuzi wa mahakama/usuhishi, zilitolewa bila kufuata utaratibu na kwamba fedha hizo ziligawanywa bila kimakosa kwa watu mbalimbali wakiwemo maafisa wa Serikali.

Video: Pongeza kwa Rais Samia
Mkuu wa kundi la Dola la Kiislamu auwawa