Mahakama moja nchini Mexico imesimamisha uhamisho wa kiongozi wa genge linalouza mihadarati nchini humo Joaquin “El Chapo” Guzman hadi Marekani baada ya watu wawili kuwasilisha kesi mahakamani ya kupinga uhamisho huo.

Mawakili wa mlanguzi huyo “El Chapo” wamepinga kuhamishwa kwake ili atumikie kifungo cha ulanguzi nchini Marekani baada ya kutoroka jela mara kadhaa akiwa nchini Mexico.

Mawakili wake wanadai kuwa hakuna ushahidi wa kumhusisha na njama ya kutoroka gerezani na wanakisia kuwa itachukuwa miaka 3 kwa kesi hizo kuamuliwa.

Awali Serikali ya Mexico ilikuwa imekubaliana na Marekani kumhamisha atumikie kifungo huko ilimradi tu asihukumiwe kifo.

Uamuzi huo wa mahakama ya juu ni pigo kwa serikali hizo mbili na vita dhidi ya ulanguzi wa mihadarati.

El Chapo alikamatwa mwezi Januari takribani miezi 6 baada ya kutoroka gerezani akitumia njia ya chini kwa chini  anakabiliwa na mashtaka ya mauaji na ulanguzi wa mihadarati nchini Marekani.

Hans van Pluijm Afichua Siri Ya Kufungwa Kwa Young Africans
Nchi iko salama - Serikali