Mahakama nchini  Ivory Coast imethibitisha kuwa Laurent Gbagbo hana nafasi ya kuwania kiti cha uras katika uchaguzi wa taifa hilo unaotarajiwa kufanyika Oktoba 31 Mwaka huu

Kwa mujibu wa mahakama ya mwanzo ya Plateau jijini Abidjan Rais huyo wa zamani wa Ivory coast amefutwa moja kwa moja kwenye orodha ya wagombea urais kutokana na hukumu dhidi yake iliyotolewa na mahakama ya Ivory Coast ya kifungo cha hadi miaka 20 jela katika kesi inayojulikana kama “wizi wa fedha katika benki kuu ya jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, BCEAO.

Wakati wa machafuko ya baada ya uchaguzi wa 2010-2011, serikali yake, ambayo ilikuwa chini ya vikwazo vya fedha, ilitumia fedha kutoka Benki Kuu ya jumuiya hiyo ya ECOWAS, BCEAO.

Baada ya kukataliwa na Tume Huru ya Uchaguzi (CEI) pamoja na mahakama ya Cote d’Ivoire, wakili wa rais huyo wa zamani anafikiria uwezekano wa kuwasilisha malalamiko yake mbele ya mahakama ya kikanda.

Young Africans waitega Simba SC
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Agosti 27, 2020