Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imetupilia mbali maombi ya zuio la uchaguzi wa Umeya katika Manispaa za Ilala na Kinondoni jijini Dar es Salaam, yaliyowasilishwa mahakamani hapo na mwananchi, Elias Nawela.

Uamuzi huo wa mahakama umeambatana na uamuzi wa kuiondoa mahakamani hapo kesi ya kupinga utaratibu wa uendeshaji wa uchaguzi huo baada ya mtoa maombi huyo kuamua kutoendelea nayo.

Uamuzi huo umetoa uhuru kwa uchaguzi wa manispaa hizo kuendelea kama ilivyokuwa imepangwa awali.

Hukumu hiyo imetolewa baada ya mtoa maombi kushindwa kuonesha uharaka wa kusikilizwa kwa maombi hayo kufuatia kushindwa kuwapatia nakala za maombi hayo upande wa wajibu waombi husika ambao ni wakurugenzi wa Manispaa za Ilala na Kinondoni.

 

Namelock Sokoine akabidhiwa mkoba wa Lowassa Monduli
Alichosema Lowassa kuhusu Viongozi wa Serikali waliomtembelea Sumaye hospitalini