Mahakama yatupilia mbali pingamizi za upande wa utetezi juu ya maelezo ya mshitakiwa wa pili Adam Kasekwa kutopokelewa na badala yake imeridhia kupokea maelezo ya mshitakiwa huyo kama kielelezo cha ushahidi upande wa mashitaka mahakamani hapo.

Baada ya maamuzi hayo yalitolewa na Jaji Kiongozi wa Mahakama hiyo Mustapha Siyani Mahakama itaendelea kumsikiliza shahidi wa kwanza kwenye kesi ya Msingi kwa upande wa mashitaka, Ramadhan Kingai ambaye hakumaliza kutoa ushahidi wake.

Akisoma uamuzi huo Jaji Mustapha Siyani ameeleza kuwa anakubaliana na Jamhuri kuwa mazingira yaliyokuwepo yana mantiki kuwa walikuwa wakiendelea na upelelezi.

Amesema kuchelewa kuhojiwa kwake kulikuwa na sababu za kisheria chini ya kifungu cha 51(1) Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.

Jaji Siyani ajitoa kesi ya mbowe
Laana ya mwanaume niliyemktaa ilivyonitesa