Mahakama Kuu ya Kenya imesitisha kutekelezwa mfumo wa usajili wa wananchi kwa njia ya alama za vidole hadi hapo sheria ya kulinda taarifa itakapopitishwa.

Mbali na zuio la utekelezaji huo, mahakama imesema kuwa kukusanya taarifa za eneo (GPS) na vinasaba (DNA) ni kinyume na katiba ya nchi hiyo.

Serikali ya Kenya imekuwa ikikusanya taarifa mbalimbali katika usajili huo ikiwa ni pamoja na alama za vidole, taarifa za familia, na eneo kamili mtu analoishi.

Wakati zoezi hilo ambalo serikali ilisema ni la lazima wale wote ambao hawatojiandikisha hawatopata huduma za msingi za serikali kama vile pasi ya kusafiria ”passport”, na cheti cha kuzaliwa.

Mahakama imezuia zoezi hilo kwa kile ilichoeleza kwamba wananchi wanaweza kujikuta katika hatari isiyorekebishika endapo taarifa zilizokusanywa zitatumiwa vibaya.

Majaji watatu wa mahakama hiyo waliamuru kusitishwa kwa mpango huo unaofahamika kama HUDUMA NAMBA hadi sheria ya kina ya kulinda taarifa zinazotolewa na wananchi upitishwe.

Waumini 20 wafariki wakigombea mafuta ya upako ya Mwamposa
Masauni atinga TAKUKURU kwa mahojiano juu ya kesi iliyomtumbua Lugola uwaziri