Kiongozi wa chama cha Kiislamu cha Ennahdha, Rached Ghannouchi, amefikishwa mbele ya mahakama ya Sousse (mashariki), kujibu tuhuma mbalimbali za utakatishaji fedha na kuchochea ghasia.

Ghannouchi, ambaye aliongoza Bunge lililosimamishwa Julai 2021 na kisha kuvunjwa na Rais Saied, awali Julai 2022 alikuwa tayari amehojiwa kama sehemu ya uchunguzi uliofunguliwa katika kesi hii iitwayo “Instalingo”.

Wanachama wengine wa Ennahdha pia wanashtakiwa kwa tuhuma za miamala ya kifedha na Instalingo, kampuni ya utengenezaji wa maudhui ya kidijitali, wakishutumiwa kulingana na vyombo vya habari vya ndani kwa kuanzisha kampeni za kashfa dhidi ya maafisa wakuu wa serikali.

Kiongozi wa chama cha Kiislamu cha Ennahdha, Rached Ghannouchi. Picha na Africanews.

Ghannouchi (81), ni mkosoaji mkubwa wa mapinduzi ya Rais Saied, ambaye alichukua mamlaka kamili mnamo Julai 25, 2021. Pia anashitakiwa katika kesi nyingine inayojulikana kama “usafirishaji wa wanajihadi” katika maeneo ya migogoro, ambayo ina imekuwa kiini cha mjadala wa kisiasa kwa miaka mingi na hivi karibuni imeibuka tena.

Chama cha Ennahdha, ambacho ni nguzo ya serikali zilizoingia madarakani tangu 2011, kinashukiwa na wakosoaji wake na sehemu ya tabaka la kisiasa kuwezesha wanajihadi hao kupigania maeneo ambayo yamekuwa na vuguvugu hilo huku Julai (2022), Mahakama iliamuru kufungiwa kwa akaunti za benki za Tunisia za Bw. Ghannouchi na dazeni kadhaa za familia yake na chama chake.

Hata hivyo, Juni 27, 2022 mamlaka ya mahakama pia ilimpiga marufuku Ghannouchi kusafiri nje ya nchi kama sehemu ya uchunguzi mwingine wa mauaji ya viongozi wawili wa mrengo wa kushoto mwaka wa 2013.

Kamati ya uokoaji 'yakuna kichwa' tishio baa la njaa
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Novemba 11, 2022Â