Tume ya Mahakama imewafukuza kazi mahakimu 11 wa Mahakama mbalimbali nchini baada ya kuwakuta na hatia kwa makosa mbalimbali ya utovu wa nidhamu na kukiuka misingi ya utumishi wa mahakama.

Akitoa taarifa hiyo jana jijini Dar es Salaam, Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman alisema kuwa Tume ilichukua uamuzi huo katika kikao kilichofanyika Agosti 18 mwaka huu kujadili na kushughulikia masuala mbalimbali ya kinidhamu.

“Tumewafukuza mahakimu wakazi wafawidhi, mahakimu wa mahakama za Mwanzo za Rombo, Temeke, Bahi na Chamwino na watumishi wengine 23. Hii ni idadi ndogo ambayo ni sawa na asilimia 0.005 ya wafanyakazi wote lakini kwa mahakama ni doa kubwa,” alisema  Jaji Mkuu.

Aidha, alisema kuwa wengine 34 walioshinda kesi za rushwa dhidi yao Mahakamani wanaendelea kujadiliwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama ili kuona kama walifanya makosa mengine ya kinidhamu.

Jaji Mkuu aliyataja baadhi ya makosa yaliyopelekea kufukuzwa kwa Mahakimu hao kuwa ni pamoja na kutumia muhuri wa mahakama kinyume cha taratibu, kuathiri utendaji wa haki kwa kumsaidia mtu kufungua kesi moja katika mahakama mbili pamoja na kufungua kesi ya mirathi bila kuwa na hati ya kifo.

 

Obama akutana na Rais wa Ufilipino aliyemtukana tusi ‘zito’
Mgodi wa Dhahabu Geita Gold Mine Watoa Milioni 444 Kwaajiri Ya Kuchangia Madawati Mkoani Geita