Wanafunzi wawili wa Chuo Kikuu cha Benue State nchini Nigeria wamelazimika kufanya mitihani yao wakiwa ndani ya vazi rasmi la bibi harusi maarufu kama shela, baada ratiba yao ya kufunga ndoa kuingiliana na ratiba ya mitihani.

Dorcas Atsea na Deborah Atoh waliamua kufanya mitihani yao katikati ya ‘presha’ ya matukio ya ndoa ambayo mbali na kuwa ya furaha huwa na changamoto kubwa ya maandalizi na utendaji, baada ya chuo kubadili kalenda iliyoingiliana na tukio lao.

Wanawake hao marafiki na wanaochukua masomo ya uandishi wa habari na utangazaji katika chuo hicho, walifika kanisani asubuhi kufunga ndoa na wenza wao lakini walipomaliza tu walielekea moja kwa moja kwenye chumba cha mitihani chuoni kwao.

Hata hivyo, wawili hao waliibadili changamoto hiyo ya kufanya maandalizi ya matukio mawili makubwa yaani ‘ndoa na mitihani ya chuo kikuu’, kuwa sehemu ya furaha zaidi.

“Niligundua ilikuwa kitu cha furaha zaidi kwa sababu nitapata vyeti viwili muhimu kwa siku moja,” Deborah aliiambia BBC.

“Tulipoingia darasani, wanafunzi wenzetu walikuwa na furaha zaidi na walipiga picha nyingi. Baada ya mtihani tulienda kwenye sherehe ya harusi ambapo tulicheza zaidi,” aliongeza.

 

Trump aitaka Urusi kujiandaa na mashambulizi
Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Aprili 12, 2018

Comments

comments