Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu, Omar Mahita amesema kuwa miongoni mwa mambo ambayo wamemshauri IGP Simon Sirro ni kukabiliana na wanasiasa ambao kama wasipodhibitiwa wanaweza kusababisha machafuko.

Ameyasema hayo mara baada ya kukamilika kwa mkutano kati ya wakuu wa Jeshi hilo wastaafu na makamishna wastaafu na Mkuu wa Jeshi hilo wa sasa IGP Simon Sirro

Mahita amesema kuwa wamemkumbusha IGP Sirro mambo mengi ikiwemo kumpa uzoefu mwingi lakini suala kubwa likiwa ni changamoto ya kuweza kukabiliana na wanasiasa ambao wasipodhibitiwa wanaweza kusababisha machafuko.

“Kwa mkakati huu tutafika kwani tumeweza kumpatia uzoefu mkubwa wa mambo mbalimbali yakiwemo ya namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za kuitendaji wakati wa kutimiza majukumu yake,”amesema Mahita

Hata hivyo, kwa upande wake IGP Simon Sirro amesema kuwa kikao hicho kilikuwa cha kawaida cha kukumbushana wajibu wa kazi zao huku suala la weledi katika utendaji wa mafunzo maalumu likijadiliwa kwa kina

Mugabe aja na mpya, ataka mageuzi yafanyike
Manchester City yaichapa Liverpool