Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF limesikitishwa na kauli iliyotolewa na golikipa wa timu ya Shupavu ya Morogoro Khalifa Mgwira baada ya kumalizika mchezo wao wa Kombe la Shirikisho la Azam ASFC dhidi ya Azam FC iliyochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro.

Wakati akifanyiwa mahojiano Mgwira alizungumza maneno yanayoashiria kuwa wamefungwa kwasababu TFF haijawapa pesa ambazo wanazitumia kwaajili ya chakula.

Utaratibu wa TFF ni kuzipatia pesa timu kabla ya kucheza mechi zao utaratibu ambao umefanyika kwa Shupavu waliolipwa pesa zao jana ikiwemo na TFF kuwaongeza fedha ya ziada mara mbili zaidi kama yalivyokuwa maombi yao.

TFF inafanya utaratibu wa kumtaka Mgwira kuthibitisha madai yake na endapo atashindwa kuthibitisha ataadhibiwa kwa mujibu wa kanuni.

TFF inasisitiza kwa wanafamilia wa mpira wa miguu kufuata taratibu katika kuwasilisha malalamiko yao kwakuwa taratibu ziko wazi.

Mengi aipa TWCC jengo lake kuendeleza ujasiriamali
Mhagama atoa ufafanuzi muungano wa mifuko ya pensheni