Saudi Arabia imesema kutokana na janga la corona itaruhusu idadi ndogo ya watu kutekeleza ibada ya Hijja mwaka huu tofauti na kawaida ambapo takriban mahujaji wapatao milioni 2 kutoka ulimwenguni kote hufika Makka kutekeleza mojawapo ya nguzo tano za Kiislamu kila mwaka.

Serikali imesema uamuzi wake unalenga kuepusha maambukizi ya virusi vya corona ambayo hutokea kwa urahisi kwenye mikusanyiko mikubwa ya watu.

Wizara inayohusika na Hajj imesema raia wa kigeni ambao wanaishi nchini Saudi Arabia wataruhusiwa kufanya hijja kubwa ambayo inatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Julai.

Tangu mwishoni mwa Februari, ufalme wa Saudi Arabia ulisimamisha shughuli za Hijja ndongo “Umrah” kwa sababu ya milipuko wa virusi vya corona.

Mashabiki, Wanachama waombwa kufika uwanjani
ARV'S kuadimika kutokana na Corona