Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nuh Mziwanda ambaye ameshawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na msaniii Shilole na mahusiano hayo kuvunjika hivi karibuni amepata majanga tena baada ya aliyekuwa mke wake na mama mtoto wake  Nawal kuolewa na mume mwingine bila ya yeye mwenyewe kudhihinisha kuwa amemuacha Nawal kwa kumpa talaka.

Kupitia mtandao wake wa Instagram Nuhu alitoa povu lakumtakia heri aliyekuwa mke wake Nawal, ameandika,

”Nimeona Nawal na hongera sana Mungu akusimamie wewe na Mumeo katika ndoa yenu pia shikamoo bwana harusi mana ulikua unanyapia kitambo sana halafu sijui ndio mana bidada sababu nyingi mradi urudi kwenu ‘kumbe mipango ya ndoa doh’ (kama movi vile ila)”. ameandika Nuh Mziwanda.

Inasemekana kuwa baada ya tukio hilo la mke wake kuolewa Nuh ameamua kuirudia dini yake ya ukristu na camera zetu zilimbamba Nuh akiwa anatoka kanisani na kumuhoji.

”Mimi na Nawal tulitengana tu, lakini baada ya hapo kumbe mwenzangu ameshaandaliwa mume wa kumuoa, mimi baada ya kugundua hilo nikaona bora nirudi kwenye dini yangu, kwa hiyo wazazi wa mke wangu walikuwa wanajua kuwa mtoto wao ananisaliti”, alisema Nuh Mziwanda

Nuh alihojiwa kama alimpa taraka Nawal ili kumruhusu kuolewa na mume mwingine Nuh alikanusha na kusema hakutoa talaka na ameshangazwa sana na kitendo hiko na kamwe hawezi kumpa talaka kwani tayari ameshaolewa na itakuwa ni kujichoresha.

“Mimi sijatoa talaka, na kufuatilia suala la talaka itakuwa kama najichoresha kwani wao wazazi wanajua kabisa kama ni mke wangu lakini wao wakaamua kumuozesha kwa mtu mwingine, kwa hiyo mimi naacha tu, mimi nitaangalia.

JPM awaunganisha Ruge na Makonda jukwaani, ‘nataka mpendane’
JPM aahidi neema nyingine Tanga baada ya mafuta, kufufua bandari