Mtangazaji maarufu, Maimartha Jesse ameingilia kati sakata la mwimbaji Ray C kurudi katika matumizi ya dawa za kulevya licha ya kudai kuachana na dawa hizo.

Maimartha amemtaka Ray C kuweka ukweli hadharani ili asaidiwe kwani anajua kuwa anatumia dawa hizo na kwamba hata yeye yuko tayari kumsaidia aachane na matumizi ya unga.

maimartha

Maimartha Jesse

“Ray C nakupenda saana…acha unayoyafanya Mimi najua kila kitu…nimejitahidi kukaa kimya nimeona siwezi….usimtese mama Rehema wala kaka tonny ….Mimi nakuomba acha ….nahitaji nikusaidie kupitia NGO Yangu ya #maihandhelp IG. #specialloveandcarefor#rayc Nitarudi na mrejesho soon! Nawapenda,” Maimartha ameandika Instagram.

Hivi karibuni, kumekuwa na taarifa pamoja na picha zinazoeleza kuwa Ray C amerudia enzi zake za kubwia ‘unga’ na kwamba ameondolewa kwenye orodha ya wanaopokea dozi maalum katika hospitali ya Mwananyamala.

Baada ya kumtimua Anne Kilango, Magufuli awasaka Mawaziri, awarekodi kwa siri
Aveva Atangaza Kamati Ya Maendeleo Ya Ujenzi Wa Uwanja Bunju