Idadi ya vifo kutokana na janga la virusi vya corona nchini China imefikia watu 304 kufikia jana usiku, baada ya watu 45 wengine kufariki dunia, Serikali ya nchi hiyo imetoa tangazo juu ya utaratibu mpya wa kuwazika waliofariki kwa kuwachoma moto.

Tume ya Afya nchini humo imesema vifo hivi vipya vilitokea katika mkoa wa Hubei, ambao ndio kitovu cha mlipuko wa virusi hivyo. Kote nchini China, kulikuwa na maambukizi mapya ya watu 2,590 jana Jumamosi na kufikisha 14,380 jumla ya idadi ya watu walioambukizwa mpaka sasa.

Janga hilo limesababisha mataifa mengi kuwahamisha raia wao huku mashirika ya ndege yakisitisha safari kwenda nchini humo.

Hatua hiyo pia inatishia kuathiri kwa kiasi kikubwa kushuka uchumi wa taifa hilo la pili kwa ukubwa kiuchumi duniani. Kumeripotiwa zaidi ya visa 130 vya maambukizi ya virusi vya corona katika karibu nchi nyingine 24 duniani.

Mambo 9 ya msingi ya kuzingatia ili kuwa dereva bora barabarani
Waumini 20 wafariki wakigombea mafuta ya upako ya Mwamposa