Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa amemuagiza Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini Mkoa wa Kigoma Mathius Mwenda kuhakikisha mradi wa maji wa Kifura Wilayani Kibondo unakamilika ifikapo Februali mwakani.

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa agizo hilo alipotembelea na kukagua mradi huo ambao unatarajia kuwanufaisha wananchi wapatao 12,095 wa kijiji cha Kifura.

Amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan analenga kuhakikisha kila mtanzania anafikiwa na huduma ya majisafi na salama, hivyo watendaji wa serikali wanapaswa kusimamia hilo.

“Mama Samia amedhamiria kupeleka Maji kwa kila Mtanzania. Anafaham jinsi akinamama, vijana na watanzania wote wanavyohangaika kutembea kwa miguu, bodaboda na baiskeli wakiwa na madumu ya maji. Kwa hiyo anafanya kila njia kuhakikisha huduma hii inamfikia kila Mtanzania,” Amesema Waziri Mkuu Majaliwa.

Awali akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi huo Meneja wa Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Kigoma Mathius Mwenda amesema mradi huo unatekelezwa na mkandarasi M/s NANGAI Engineering and Contractors Co. Ltd kwa Gharama ya EUR 880,256.54 sawa na shilingi Bilioni 2,405,741,123.83 za Kitanzania.

Aidha fedha yote ya utekelezaji wa mradi ipo, hakuna shaka mashaka kwamba mradi huo utakamilika kwa wakati.

Sambamba na hayo yote Mkenda amemuhakikishia Waziri Mkuu kuwa mradi huo utakamilika kwa wakati. Mradi wa maji Kifura ni moja ya miradi ambayo inatekelezwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Ubelgiji mkoani Kigoma.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Septemba 19, 2021
Waziri Ummy atoa agizo kwa Muhandisi wa Halmashauri ya Kisarawe