Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameapa kupambana na ufisadi na upotevu wa mapato ya serikali hadi dakika ya mwisho.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam,  alipokuwa akifunga maadhimisho ya miaka 20 ya Dayosisi ya Pwani ya kanisa la African Inland Church (AIC) kwa niaba ya Rais John Magufuli.

“Nia yetu ni kuhakikisha kila kinachopaswa kukusanywa kama mapato ya nchi, kikusanywe na kutumike kwa masuala ya msingi kwa ustawi wa Watanzania wote na sio kwa watu wachache, ” Waziri Mkuu alisema.

Aidha, aliwaomba watanzania wa imani zote wawaombee ili waweze kufanikiwa.

“Wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi, bali muovu atawalapo watu huugua,” Majaliwa alinukuu Biblia katika Kitabu cha Mithali Sura ya 29.

Huku ndiko yalikopelekwa Makontena Yaliyokwepa Kodi, Kova kutoa Tamko leo
Azam Wafafanua Kuhusu Sakata la Kupotea Makontena Bandarini Yaliyodaiwa Kuwa Ya Bakhresa