Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameendesha hafla ya uchangishaji wa papo hapo na kufanikiwa kupata shil. milioni 138.26 kwaajili ya ujenzi wa shule mpya wilayani Ruangwa.

Hatua hiyo imetokana na wingi wa wanafunzi waliofaulu mtihani wa Darasa la saba na kuchaguliwa kuingia kidato cha kwanza lakini walikosa nafasi kulingana na uhaba wa shule za sekondari wilayani humo.

“Katika kikao cha Halmashauri ya wilaya cha hivi karibuni, ilionekana kuna haja yakujenga shule mpya ya sekondari ili kukabiliana na wingi wa watoto waliofaulu mtihani wa darasa la saba na kuchaguliwa kuingia kidato cha kwanza, tunawashukuru sana wenzetu waliojitolea maeneo yao bure ili shule ijengwe haraka”amesema Majaliwa.

Hafla hiyo imefanyika katika mkutano wa hadhara, uliofanyika mjini Ruangwa,ambapo Waziri Mkuu amefanikisha kupatikana kwa fedha milioni 120.65 na mifuko 550 ya saruji na mabati 360, vitu vyote vina thamani ya shil. milioni 17.61 ambavyo vitatumika kujenga madarasa manne.

 

 

Nikki Mbishi aikashifu Lugha ya kingereza
Nikki Mbishi: Nafsi ya Chidi Benz haiko tayari kusaidiwa kuacha Ngada