Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amefanya ukaguzi wa matengenezo ya makazi ya muda yatakayotumiwa na makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan atakapohamia Dodoma.

Akitoa taarifa ya ujenzi huo, Waziri wa Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Wenye Ulemavu na Vijana, Jenista Mhagama amesema kuwa kikosi kazi kimebaini mahali alipokuwa akiishi zamani si sahihi kwa makazi ya kudumu.

“Pale palikuwa panafaa kwaajili ya ziara ya kikazi alipokuwa akija Dodoma, kwa hiyo tumeamua kufanya ukarabati hapa Kilimani ili aweze kuishi kwa viwango vinavyostahili,”amesema Mhagama

Amesema kuwa kazi ya ukarabati wa matengenezo hayo itagharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.5, wakati kazi ya kutenganisha watumishi na wasaidizi wa makamu wa Rais itagharimu kiasi cha Sh. 680 milioni.

Naye Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo (TBA) mkoa wa Dodoma, Steven Simba anayesimamia ujenzi huo amesema kuwa wanatarajia kumaliza ukarabati huo kabla ya Desemba 30 mwaka huu.

 

Mhagama aitaka MIVARF kuongeza thamani ya biashara
Chadema: Njaa na usaliti vinawafanya wahame