Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amefungua kiwanja kipya cha Taifa cha mchezo wa Baseball na kuzindua mashindano ya Taifa ya Baseball nchini.

Amewaagiza viongozi wa Wizara ya Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni na Ofisi ya Rais-TAMISEMI waone umuhimu wa kuuendeleza mchezo huo.

Ameyasema hayo mara baada ya kufungua kiwanja cha Baseball katika shule ya Sekondari ya Azania, jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa iwapo mchezo huo utaratibiwa vizuri na kuingizwa katika michezo UMISETA na UMITASHUMTA utaleta tija kwa wanafunzi wanaoucheza nchini.

Aidha, ameongeza kuwa thamani ya uwanja huo ni takribani Dola za Kimarekani 80.234 ambazo zimetolewa kwa msaada kutoka Serikali ya Japani.

Majaliwa ameongeza kuwa anaishukuru Serikali ya Japan na amefarijika kwa dhamira yao ya kuunga mkono utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi CCM 2015-2020 hususan ibara ya 161.

Kwa upande wake, balozi wa Japan nchini, Shinichi Goto amesema nchini Japan mchezo huo pia unasaidia katika kuwajenga vijana kukua kinidhamu na kujiamini.

 

Benki ya TPB yaandaa mkutano wa mabenki ya Akiba Afrika Mashariki
Rusia yatishia kuendelea na mpango wake wa makombora