Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amegawa kadi za matibabu kwa wazee 280 wa Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara, kadi hizo zitawawezesha wazee hao kutibiwa bure.

Amesema Serikali imedhamiria kuboresha huduma za afya kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kutoa matibabu bure kwa wazee walio na umri wa kuanzia miaka 60.

Amekabidhi kadi hizo alipotembelea mradi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Serengeti, inayojengwa katika mji wa Mugumu.

Aidha, amesema kuwa Serikali kwa kushirikiana na Halmashauri ya wilaya ya Serengeti itakamilisha ujenzi wa hospitali hiyo, itakayokuwa na uwezo wa kuwahudumia wakazi wa wilaya hiyo na wageni.

Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya hiyo, Nurdin Babu amesema kuwa tangu mwaka 1974 wilaya hiyo ilipoanzishwa hadi sasa haina hospitali ya wilaya na wakazi wake wanatibiwa katika hospitali teule ya Nyerere inayomilikiwa na kanisa la Mennonite Tanzania.

 

 

Mtoto ajinyonga kwa kukataliwa ombi lake
Jaji Mutungi avifunda vyama vya siasa