Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema kuwa atamuita Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho, Hassani Jarufo amueleze  sababu za kucheleweshwa kwa malipo ya wakulima kinyume na agizo lililo tolewa na Serikali.

Ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara na wakulima wa korosho Wilayani Nachingwea Mkoani Lindi, Majaliwa amesema alishatoa maelekezo tangu mwezi Aprili wanunuzi wa korosho watoe asilimia 25 ya malipo wanayotaka ili kuepuka madalali kuingilia kati biashara hiyo.

“Niliagiza wanunuzi waje na Bond (dhamana), waziweke benki ili waingiziwe kwenye mnada, kwa maana hiyo ukimalizika, benki inakata fedha husika na kuingiza kwenye chama cha wakulima”amesema Majaliwa.

Hata hivyo ametoa agizo hilo mara baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wakulima wa korosho kucheleweshewa malipo yao.

T.I na Tiny wapigana chini, Mayweather atajwa kuwa chanzo
BoT yadaiwa shilingi 3.5 bilioni