Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameishukuru Serikali ya Cuba kwa kutambua na kuthamini mchango mkubwa uliotolewa na mashujaa wa ukombozi wa Bara la Afrika, akiwemo Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere kwa kuwajengea mnara wa kumbukumbu.

Mnara huo umejengwa katika Manispaa ya Playa jijini Havana kwenye eneo maalumu la makumbusho ya mashujaa hao walioshiriki katika ukombozi wa Afrika, ambapo  zimewekwa sanamu zao pamoja na maelezo mafupi ya historia zao na nchi wanazotoka.

Waziri Mkuu alifanya ziara na kuweka shada la maua katika mnara huo uliozungukwa na sanamu za mashajuaa wa Bara la Afrika na kuonyeshwa sehemu itakayowekwa sanamu ya Mwl. Nyerere.

Aidha, Majaliwa ameishukuru Serikali ya Cuba kwa kujenga makumbusho ya mashujaa hao na kwamba Serikali ya Tanzania itashirikiana na Cuba kuhakikisha kuwa sanamu ya Mwl. Nyerere inawekwa katika sehemu iliyotengwa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Instuto Cubano De Amistad Con El Pueblo (Taasisi ya Ushirikiano wa Cuba na Nchi Marafiki), Jose’ Prieto Cintado amesema kuwa mnara huo umejengwa kwa lengo la kutambua thamani na umuhimu wa viongozi hao.

 

‘Seduce Me’ ya Ali Kiba yavunja rekodi Afrika Mashariki
Video: Mayweather alivyomzima McGregor kwa KO