Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameiagiza halmashauri ya Kilosa kulipa deni la shilingi milioni 210 kwa Halmashauri ya Gairo fedha ambazo zilichukuliwa wakati wilaya hiyo ilikuwa haijafungua akaunti.

Aidha, Majaliwa ametoa agizo hilo alipokuwa akizungumza na viongozi wa mkoa wa Morogoro, Wilaya ya Gairo na watumishi wa Halmashauri ya hiyo mara baada ya kupokea taarifa ya mkoa na wilaya katika kikao hicho.

“Kilosa ni lazima wazilipe hizo fedha. Katibu Tawala simamia zoezi hilo na kama watachelewa, uzikate moja kwa moja kwenye fedha yao wanayoletewa kutoka Ofisi ya Rais (TAMISEMI). nataka nipewe taarifa ya maamuzi hayo kabla Juni haijaisha,” amesema Majaliwa.

Hata hivyo, akitoa taarifa ya wilaya hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe amesema wanaidai Halmashauri ya Kilosa sh. 233,228,679 ambazo ziliingizwa huko wakati wilaya hiyo  inaanzishwa na hawakuwa wamefungua akaunti ya wilaya.

 

Beckham awachanganya wazazi kwa busu alilompa mwanae wa kike akiwa Afrika
Picha mpya za Beyonce zazua gumzo, mashabiki waunganisha matukio