Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekagua maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa yanayotarajiwa kufanyika Kitaifa Mkoani Dodoma Julai 25, 2022, kwenye viwanja vya Mashujaa.

Waziri Mkuu amefanya ukaguzi huo hii leo Juali 23, 2022 akiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene, ambapo mgeni rasmi anatazamiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,,akijadiliana jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene wakati akikagua  maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa yatakayo fanyika Kitaifa Mkoani Dodoma Julai 25, 2022.

Julai 21, 2022 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka alitembelea kukagua maandalizi hayo na kuzungumza na Waandishi wa habari ambapo aliwataka Wakazi wa Mkoa huo kujiandaa ili kushiriki siku hiyo ya Mashujaa itakayofanyika katika eneo hilo Kitaifa.

“Sherehe za mashujaa kitaifa zinafanyika Dodoma na Rais Samia atakuwa Mgeni rasmi siku hiyo tujiandae kujumuika na Rais wetu maana hii ni heshima kubwa sana kwetu Wanadodoma hivyo tumejiandaa vizuri kuipokea siku hiyo,” alisema Mtaka.

Maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa yatakayo fanyika Kitaifa Julai 25, 2022, kwenye viwanja vya Mashujaa jijini Dodoma. 

17 wauawa na majambazi, wamo Polisi watano
Wawili wauawa tukio la ujambazi wa kutumia Silaha