Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amempa siku 18 Mkandarasi wa umeme kwenye kiwanda cha Kiluwa Steel Group awe amemaliza kazi ya kuweka umeme wa msongo mkubwa ili kiwanda hicho kianze kazi.

Majaliwa ametoa agizo hilo leo Novemba 19, 2016 wakati akizungumza na wananchi na viongozi mbalimbali wa Serikali na wa Mkoa wa Pwani waliofika kiwandani hapo eneo la Mlandizi wakati akikagua utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa Julai 12, mwaka huu alipozuru kiwanda kwa mara ya kwanza.

Majaliwa amesema alipofika hapo kwa mara ya kwanza aliagiza itengenezwe njia ya reli kutoka njia panda ya reli ya kati, lakini pia aliagiza uwekwe umeme wa msongo mkubwa ili kiwanda kiweze kuanza uzalishaji mapema mwakani, hivyo amefarijika kukuta maagizo haya yametekelezwa kwa kiasi kikubwa isipokuwa agizo la umema.

“Mkandarasi ameomba siku 14, nimempa hadi tarehe 7 Desemba ahakikishe umeme unafanya kazi kwa kiwango kinachotakiwa. Sasa hivi wameanza test lakini muda ili transforma iweze kuhimili mzigo mkubwa… hili ni suala la kitaalamu kwa hiyo tuwape muda.” – Majaliwa

 

 

 

 

 

Sakata la Mchezaji Langa Lesse Bercy Wa Jamhuri ya Congo laishtua tena TFF
Video: Kiwanda cha dawa za binadamu chapigwa faini Sh. Mil. 20