Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amememuagiza mkaguzi mkuu wa Serikali  kuchunguza hali ya upatikanaji wa dawa katika zahanati na kituo cha afya cha mjini Gairo, mkoani Morogoro.

Ameyasema hayo wakati akihutubia wakazi wa mji wa Gairo na vitongoji vyake kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Gairo ‘A’ ambapo amesema hajaridhishwa na maelezo ya mganga mkuu wa hospitali hiyo ya upatikanaji wa dawa.

“Sasa ni lazima nilete mkaguzi kutoka ofisi yangu ili tupate picha halisi kama dawa zinazoletwa zinafika, na kama zinafika zinatumikaje. huyu mkaguzi atakuja kukukagua wewe mwenyewe na kwenye zahanati zako,” amesema Majaliwa.

Hata hivyo, amesema kuwa katika mkutano wake na watumishi Serikali amewaeleza kuwa wao ni maafisa wa kukaa ofisini tu na wala si kwenda sehemu yeyote kujua hali ikoje ya upatikanaji wa dawa.

Lowassa ampa tano Rais Magufuli, ataka watanzania wamuache apitishe fagio
Fainali ya UEFA yasababisha mashabiki 1000 wa mpira kujeruhiwa