Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amepiga marufuku tabia ya wakandarasi wa miradi ya maji kuagiza mabomba nje ya nchi wakati kuna mabomba yanayozalishwa hapa nchini tena kwa ubora.

Hivyo amewataka wakandarasi hao kutumia mabomba yanayotengenezwa ndani ya nchi.

“Niwatake wakandarasi tuendelee kutumia mabomba ya ndani ili kuendelea kutoa sapoti kwa wawekezaji hawa,”amesema

“Kuna mradi wa kusambaza maji katikati ya mji wa Sh14 bilion ambao upo hatua za manunuzi, mkurugenzi wa Mwauwasa simamia hilo wakandarasi wanunue mabomba kiwanda hiki,” amesema  Waziri

Ameyasema hayo Februari 20  wakati akiweka jiwe la msingi katika kiwanda cha kuzalisha mabomba cha Mwanza Plastics eneo la Nyamhongolo wilayani Ilemela Mwanza.

Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, John Charles amesema kiwanda hicho chenye wafanyakazi 15 ambao ni wazawa wenye ajira za kudumu na watatu kutoka nje ya nchi, kilianza mwaka 2008 kwa kutengeneza plastiki na vikombe.

Amesema wanakabiliwa na uhaba wa umeme wa kutosha kwani wakati mwingine unakosa nguvu na miundombinu ya barabara hivyo kuongeza gharama za uzalishaji.

Kutokana na hayo Waziri alimwagiza mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela John Wanga kuhakikisha maeneo yote ya uwekezaji miundombinu yote muhimmu inafika.

Aadhibiwa kupiga deki ofisi ya mtendaji kwa miezi mitatu
Takataka zaua watu 17, zazika nyumba