Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amepokea msaada wa Dola za Marekani 33,000 sawa na Shilingi Milioni 71 za Kitanzania kutoka kwa Umoja wa Makampuni ya Kuwait kwa ajili ya wahanga wa tetemeko la ardhi  lililotokea mkoani kagera.

Msaada huo umekabidhiwa kwa Waziri Mkuu na Balozi wa Kuwait nchini Jasem Al-Najem leo Novemba 9, 2016. Balozi huyo amesema kuwa msaada huo ni mchango kutoka kwa Mwenyekiti wa umoja wa makampuni ya Foud Alghanim, Foud Alghanim aishiye Kuwait kwa sababu wameguswa na maafa yalitokea mkoani Kagera Septemba 10, mwaka huu.

Balozi huyo amesema kuwa wanatambua kuwa kazi ya kurejesha huduma kwa wananchi ni kubwa na Serikali peke yake haiwezi kubeba mzigo wa kukarabati miundombinu na majengo ya ofisi na makazi ili kuurejesha mkoa huo katika hali yale ya kawaida.

Akitoa shukrani kwa Balozi baada kupokea msaada huo Waziri Mkuu, Majaliwa amesema Serikali ya Tanzania imeguswa na moyo wa upendo kutoka kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Makampuni ya Fouad, Alghanim na wenzake na amemhakikishia Balozi huyo  kuwa Serikali itahakikisha mchango huo unafikishwa Kagera kwa walengwa.

Video: Machinga watakiwa wasiishi kwa mazoea
Wafanyabiashara wa viumbe pori hai wamlilia Rais Magufuli