Kijana Majaliwa Jackson ambaye aliwaokoa abiria 24 wa ajali ya ndege ya Kampuni Precision Air ya Novemba 6, 2022 mjini Bukoba Mkoani Kagera, amefika Bungeni jijini Dodoma akiongozana na askari kutoka Jeshi la Zimamoto, Shaban Mkingilo na kupongezwa na Bunge kwa ujasiri wake.

Pongezi hizo, zimetolewa na Spika wa Bunge la Jmhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson hii leo Novemba 11, 2022 ambapo amemshukuru Majaliwa kwa kazi nzuri aliyoifanya nakusema Bunge linatambua juhudi kubwa zilizofanywa na kijana huyo katika ajali hiyo iliyosababisha vifo vya watu 19 na wengine 24 kujeruhiwa.

Majaliwa Jackson (kulia).

Aidha, Wabunge wamechangia shujaa Majaliwa kiasi cha shilingi Million 5 kumpongeza kwa ushujaa aliouonesha huku Spika Tulia akisema, “Navishukuru vyombo vya ulinzi na usalama, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa hatua zote alizozichukua pamoja na kuagiza kijana huyo kuajiriwa na Jeshi la Uokoaji.”

Aidha, Mbunge wa Mkalama (CCM), Francis Mtinga amempongeza baba wa Majaliwa kwa malezi mazuri ambayo amemlea na kumfanya kuwa shupavu huku Spika Tulia akimpongeza mama wa Majaliwa kwa kumlea na kumpa ujasiri wa kujiamini.

Shambilizi la bomu Ukraine lauwa watu sita
Sadio Mane atajwa safari ya QATAR