Katika harakati za kudumisha haki za watoto na kuhakikisha wanapata elimu, Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa amesisitiza na kuzitaka halmashauri zote nchini kuhakikisha kuna shule za msingi zenye madarasa ya awali na pia kuwepo kwa shule zenye kidato cha tano na sita.

Akiwa kama kiongozi na mfano mzuri katika jamii, Majaliwa amezindua madarasa manne ya kidato cha tano katika shule ya sekondari ya Nyehunge wilayani Sengerema.

Majaliwa ametoa kauli hiyo Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza katika ziara yake ya siku saba mkoani Mwanza ambapo amewasisitiza walimu wasijiingize katika masuala ya michango bali wajikite na taaluma.

Elimu bora ni pamoja na miundombinu bora, wanafunzi wengi vijijini hawafanyi vizuri katika elimu kutokana na miundombinu mibovu, Tanzania ina sera nyingi zinazozingatia kuboresha elimu bora.

Tatizo kubwa linaloshusha ustawi wa elimu bora ni miundombinu mibovu, shule nyingi zinachangamoto ikiwemo uhaba wa madarasa, uhaba wa samani, uhaba wa waalimu hasa katika shule zilizo vijijini, uhaba wa hifadhi nzuri za walimu na mengine mengi.

Hivyo kama Serikali ichunguze namna ambavyo inaweza kutatua tatizo la elimu kwa kurekebisha miundo mbinu kwanza, kwani tatizo la wanafunzi kusomea chini ya mti bado lipo katika sehemu kubwa ya nchi, hasa katika mkoa wa Mtwara ambao elimu yao bado ipo chini na hizo ndio changamoto kubwa zinazowakabili.

 

Diamond amjibu Zari, 'hujaacha tobo uliloniachia ni bonge la tundu'
Video: Papii Kocha ahuzunisha dunia na wimbo wake mpya ''Waambie''