Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa mwezi mmoja kwa watumishi waliohamishiwa wilaya mpya ya Kibiti mkoani Pwani kuripoti katika kituo chao cha kazi na watakaoshindwa kutekeleza watakuwa wamejifukuzisha kazi.

Majaliwa amesema hayo leo Septemba 28, 2016 wakati akizungumza na watumishi wa wilaya hiyo katika ziara yake ya kukagua shughuli za maendeleo, utendaji wa serikali na kutoa msimamo wa serikali  kuhusu utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku ambapo amesema mtumishi yeyote aliyehamishiwa wilaya hiyo ambaye anaishi nje ya Kibiti anatakiwa arudi na kuishi kwenye makao makuu ya wilaya na si vinginevyo.

“Tayari nimemuagiza ndugu Zuberi Samatabu  Katibu Tawala wa mkoa wa Pwani kuhakikisha anasimamia watumishi wote wa wilaya hiyo wanaoishi nje ya wilaya hiyo  waishi Kibiti na si Ikwiriri,” amesema.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo kufuatia taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo Alvera Ndabagoye ambaye alimueleza Waziri Mkuu  kuwa ni watumishi wanane pekee kati ya  74  waliopangiwa kufanya kazi kwenye wilaya hiyo wameripoti  katika kituo cha kaz

Majaliwa amesema ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa nyumba za watumishi amemuagiza Mkuu wa  Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kuzungumza na watendaji wa mifuko ya hifadhi  ya jamii kwenda wilayani huko kuwekeza katika miradi ya ujenzi wa nyumba za watumishi.

Waziri Mkuu pia amewataka madiwani wa halmashauri hiyo wawe wakali katika kusimamia miradi ya maendeleo na kuacha tabia ya kuomba omba kwa wakuu wa idara ili kuepuka kujishushia hadhi zao na kupelekea kuhujumiwa kwa miradi mbalimbali ya jamii

Aidha, amewataka viongozi wa wilaya hiyo kutengeneza mazingira ya kukaribisha wawekezaji na wahakikishe kwamba uwekezaji utakaofanyika hausababishi migogoro ya ardhi kwa wananchi.

Majaliwa amewahamasisha wananchi kuhakikisha wanapeleka watoto shule kwa maana Serikali imebeba mzigo wote wa gharama za ada na uendeshaji wa shule hizo. Alisisitiza kuwa njia pekee na ya haraka kuondoa umaskini ni kusomesha watoto

halmashauri zote nchini zimetakiwa kutumia mfumo wa kieletroniki katika ukasanyaji wa mapoto ili kuziba mianya ya  uvujaji mapato haswa ya maliasili.

Picha: Serengeti Boys Walipowasili Mjini Brazzaville
Picha: Waziri Mkuu akihutubia Wananchi Kibiti