Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, amewaonya wakazi wa Ruangwa wanaokata miti kwenye misitu waache mara moja ili kuokoa ardhi chepechepe waliyokuwa nayo.

Ameyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara na wakazi wa vijiji mbalimbali vya Wilaya hiyo ambao walifika Ruangwa mjini, amesema kuwa ukataji miti unafanywa na watu wanaoanzisha mashamba ya ufuta ambao wameamua kulima karibu na vyanzo vya maji hali iliyosababisha maji yakauke kwenye maeneo mengi.

“Kilimo cha ufuta kimekuwa balaa,sasa hivi hakuna maji sababu ya ukataji miti ovyo. mfano mzuri mto Mbwemkuru ambao ulikuwa uanatiririsha maji mwaka mzima,umegeuka kuwa mto wa msimu na chanzo ni ukataji miti”amesema Majaliwa.

Hata hivyo, Majaliwa amesema kuwa wataalamu wataanza kufanya utafiti ili kubaini maji yako umbali gani kwenda ardhini  kabla ya kuanza kuchimba visima hivyo.

Magufuli atangaza neema tena
Batshuayi Kurudi Ufaransa