Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, amewataka wakuu wa Idara kwenye Halmashauri za Wilaya na Manispaa nchini,wasaidie kutoa utaalam wao badala ya kupingana na Madiwani ili waweze kuleta maendeleo kwa wananchi.

Aidha, amewataka madiwani wasikilize ushauri wa kitaalamu unaotolewa na wakuu wa Idara katika utekelezaji wa miradi iliyotolewa na Halmashauri.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Mabada,viongozi na watendaji wa  Mkoa wa Ruvuma  akiwa katika ziara yake ya siku ya pili Mkoani humo.

”Wakuu wa Idara nyie ni washauri, tumieni taaluma zenu kutoa ushauri,semeni bila woga pale inapobidi,”amesema Majaliwa,

Majaliwa amesema kuwa Serikali iko makini katika ukusanyaji mapato na matumizi kwa kila senti  inayokusanywa na amewataka kila mmoja aongeze juhudi katika ukusanyaji mapato na amepiga marufuku matumizi holela ya fedha za umma.

Hata hivyo, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwakumbusha watumishi wa umma wajibu wao wa kuwahudumia watanzania bila kujali dini,itikadi,kabila au hali zao na kusisitiza kuwa Serikali haitamuonea mtumishi yeyote ambaye anatimiza wajibu wake.

Jaffo aunda kamati ya uchunguzi hospitali ya Mkuranga
Fonte Aomba Kuondoka St Marries Stadium