Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Kilimo itenge fedha katika bajeti yake kwa ajili ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania TARI, kituo Mlingano ili kupanua eneo la uzalishaji miche kwa kununua vitendea kazi yakiwemo matrekta.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo wakati wa ukaguzi wa kitalu cha miche ya mkonge cha TARI Mlingano kilichopo wilayani Muheza mkoani Tanga na kufungua zoezi la ugawaji wa miche kwa wakulima wa zao hilo.

Aidha, Waziri Mkuu ameiagiza Wizara ya Kilimo ifanye mapitio ya kodi na tozo zote zilizopo katika zao la mkonge kwa lengo la kubaini ni zipi zenye manufaa kwa wadau na Taifa na kuainisha zisizokuwa na tija ili zifanyiwe mchakato wa kuondolewa.

Amesema kituo cha TARI Mlingano kinatakiwa kijikite katika kufanya utafiti wa mbegu bora pamoja na dawa za kudhibiti magonjwa katika zao hilo, na suala la uzalishaji mbegu lifaywe kwa ushirikiano katika kituo hicho na wadau wa zao hilo.

Aidha, Waziri Majaiwa ameziagiza halmashauri zinazolima mkonge nchini pamoja na wakulima wakubwa wa mkonge kutenga ekari 10, kwa ajili ya kuanzisha vitalu vya kuzalisha miche ya mkonge ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa miche ya mkonge.

Haya hapa matarajio ya Chikwende Simba SC
Pitso Mosimane amtema Geraldo da Costa