Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali itahakikisha wananchi katika vijiji vyote nchini wanapata huduma ya maji safi na salama wakiwemo na wa jimbo la Bumbuli.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Mponde jimbo la Bumbuli, Lushoto.

Pia, Waziri Mkuu amemuagiza Mhandisi wa Maji wa Halmashauri ya Bumbuli, wilayani Lushoto, Charles Boy afanye utafiti na kubainisha vijiji vyenye shida ya maji Bumbuli.

Amesema kuwa baada ya kuvibaini vijiji hivyo, anatakiwa aweke mpango wa kuhakikisha navyo vinapata huduma ya maji safi ili kuwaondolea wananchi tatizo hilo la ukosefu wa maji.

“Serikali kupitia Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo kichwani, itahakikisha wananchi katika maeneo yote nchini wanapata huduma ya maji safi na salama.”amesema Majaliwa

Hata hivyo, ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ina mikakati mizuri inayolenga kumaliza tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo yote yenye changamoto hiyo nchini.

 

Unafikiria Kubadili Kazi? Ishara 6 za Kuzingatia
Tafiti zasaidia kupatikana kwa utatuzi wa changamoto sekta ya kilimo

Comments

comments