Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekabidhi magari mawili kwa ajili ya matumizi ya Jeshi la Polisi mkoa wa Lindi yatakayowezesha askari kutoa huduma katika maeneo ya Mkoa huo.

Amekabidhi magari hayo jana Jumapili, Februari 21, 2021 baada ya kuzungumza na wananchi katika kituo cha Polisi Mtama ambako makabidhiano hayo yalifanyika.

Magari yaliyokabidhiwa ni Toyota Land Cruiser Pickup yenye namba za usajili PT 2615 na Toyota Land Cruiser V6 lenye namba za usajili PT 4378.

Kati ya magari hayo gari moja TP 4378 ni kwa ajili ya ofisi ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Lindi na gari lingine PT 2615 ni kwa ajili ya kituo cha polisi cha Mtama.

Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kutoa vitendea kazi kwa jeshi la polisi kadiri inavyowezekana ili kuwawezesha askari nchini kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Akizungumza baada ya kupokea magari hayo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Lindi Mtatiro Kitinkwi alisema magari hayo yatawezesha shughuli za doria kufanyika kwa uhakika.

Gor Mahia wamchapa mwamuzi ugenini
Manara: Siitanii tena Young Africans