Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametangaza vita na watu wanaoteka watoto na kudai fedha na wakati mwingine kuwaua watoto hao.

Ameyasema hayo wakati wa kikao na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kigoma alipoanza ziara ya siku nne mkoani humo.

Amesema kuwa ameamua kulivalia njuga suala hilo na masuala ya ujambazi ambayo kwa kiasi kikubwa yanafanywa na wageni kutoka nje wilaya ya Kibondo na Kakonko.

Katika kuhakikisha anaanza utekelezaji kwa vitendo wa suala hilo, anafanya ziara yake mkoani Kigoma kwa njia ya barabara ambako atapitia maeneo yenye matatizo hayo wakati akielekea mkoani Kagera.

Aidha, amesema kuwa pamoja na utekaji wa watoto, matumizi ya silaha pia ni makubwa katika maeneo hayo hivyo anaanza mkakati wake kwa kuzungumza na wakimbizi wa Burundi katika kambi ya Nduta Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma na kwamba vitendo hivyo lazima vikomeshwe.

Akizungumzia kilimo cha michikichi, amesema kuwa serikali imeamua Kigoma kuwa mkoa kiongozi katika kilimo cha michikichi na ziara yake inafuatilia maagizo yaliyotolewa katika utekelezaji wa mikakati mbali mbali ya kuinua zao hilo.

Wananchi wa Nkuyu wazungumzia umuhimu wa Kokoa Kyela
Chid Benz adai muziki umekuwa hatari, ‘It’s either uko Wasafi au Wachafu’

Comments

comments