Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amezindua mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa kwa mwaka 2023, zilizofanyika katika uwanja wa Chama Cha Mapinduzi – CCM, wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.

Mbio hizo, zimezinduliwa hii leo Aprili Mosi, 2023 ambapo viongozi kadhaa walihudhuria zoezi hilo akiwemo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Prof. Joyce Ndalichako.

Wengine ni Katibu Mkuu Ofisi wa Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Prof. Jamali Katundu na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas Ahmed na Wananchi.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Mtwara wakati alipozindua Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 katika uwanja wa CCM Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara, Aprili Mosi, 2023.

Tujenge mazoea ya kusoma Vitabu: Mchungaji Msigwa
Urusi yatwaa Uenyekiti Baraza la Usalama Umoja wa Mataifa