Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amezindua mfumo wa tiketi za kielektroniki za kuingialia uwanja wa Taifa.

Uzinduzi huo umefanyika jana Septemba 25 2016 kabla ya mchezo kati ya Wabunge wapenzi wa Yanga dhidi ya Wabunge wapenzi wa Sima,  ambapo Waziri Mkuu amesema kuwa  mfumo huo uko vizuri na unatakiwa kuendelea kutumika.

Majaliwa amesema ameridhishwa na mfumo huo na unatakiwa kutumika katika viwanja vyote vya michezo hasa huo uwanja wa Taifa ili kuziwezesha timu na nchi kupata mapato.

Tayari mfumo huo umeanza kutumika jana katika pambano la Wabunge Yanga na Simba ambalo lilitanguliwa na pambano la wasanii wa Bongo Fleva dhidi ya wasanii wa Bongo Movie ikiwa ni kwa ajili ya kuchangia waathirika wa tetemeko la ardhi Kagera.

Pambano hilo liliingiza shilingi milioni 187.

 

Griezmann: Bado Ninamuhitaji Diego Simeone
Kevin de Bruyne Aiweka Majaribuni Man City