Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema kuwa Halmashauri zote zinazozalisha mkaa Nchini zinatakiwa kuanzisha mashamba ya miti  kwa ajili ya kupata nishati hiyo,

Hayo yamesemwa  na Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jummanne Maghembe alipomwakilisha wakati wa ufunguzi wa warsha ya kujadili mikakati ya kupunguza matumizi ya mkaa iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dar es Salaam.

Amezitaka Halmashauri zote nchini kuandaa mwongozo wa uzalishaji, matumizi na biashara ya mkaa katika mashamba yatakayoanzishwa na kuagiza program za kupanda miti zifanyike wakati wa msimu wa mvua ili kuhakikisha miti yote inapona.

Aidha, amesisitiza kuwa kila mfanayabiashara wa mkaa ahakikishe lazima  ana shamba la miti kwa ajili ya nishati ya mkaa na vibali vya biashara hiyo vitolewe kwa masharti.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira, January Makamba alisema kuwa  Ofisi ya Makamu wa Rais itashirikiana bega kwa bega na Wadau ili kupunguza utumiaji wa matumizi ya mkaa. Alitanabaisha kuwa Ofisi yake imeandaa shindano la kutafuta mkaa mbadala na mshindi wa kwanza atapata milioni 300.

Makinda: Mabadiliko sheria ya ndoa ni muhimu
Rais Lungu: Muda wa siasa umekwisha, sasa ni kazi tu