Waziri mkuu Kassim Majaliwa ameiagiza idara ya uhamiaji mkoani Mwanza kuzuia kwa muda hati za kusafiria za raia saba wa Korea wanaojenga meli ya MV Mwanza “Hapa kazi tu” ili wasiondoke nchini hadi wakamilishe ujenzi wa meli hiyo.

Hatua hiyo imekuja baada ya waziri mkuu kufanya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa meli hiyo na kugundua ukiukwaji wa makubaliano ya mkataba wa ujenzi wa meli hiyo Jumamosi, Mei 7, 2022 katika eneo la Mwanza South, wilaya ya Nyamagana, jijini Mwanza.

Wenye pasi hizo ni Meneja wa mradi, Dong Myung, na wasaidizi wake Kyungan Choi na Bw. Khuh Yun.

Miongoni mwa maeneo ambayo waziri mkuu amebaini ukiukwaji wa mkataba ni pamoja na kampuni ya Korea ya Gas Entec iliyo na jukumu la kujenga meli hiyo kuuza sehemu ya jukumu la ujenzi kwa kampuni nyingine sababu iliyochangia ujenzi wa meli hiyo kufikia asilimia 65 pekee badala ya asilimia 95 iliyotarajiwa kwa mujibu wa makubaliano ya muda uliotolewa wa kukamilisha kazi hiyo.

Waziri Mkuu Kassim Majolica akita taarifa ya Ukaguzi

“Nimemwagiza Afisa Uhamiaji wa Mkoa akamate pasi zao mara moja na ahakikishe hakuna mtu anatoka nje ya mkoa huu hadi hii kazi ikamilike. Nimeambiwa wako saba, lakini hapa wako watatu. Watafuteni hao wengine wako wapi.”

Waziri Mkuu ambaye yuko mkoani Mwanza kwa ziara ya siku moja, amesema Serikali imeshalipa asilimia 80 ya gharama za ujenzi wa meli hiyo lakini kazi iliyofanyika kwa mujibu wa mkataba ni asilimia 65 tu. Amesema taarifa alizonazo zinaonesha kuwa wafanyakazi walikuwa 118 lakini sasa wamebakia 22 tu.

“Nimeingia ndani kukagua kazi ya ujenzi lakini sijaridhika nayo. Katika maelezo yao nimebaini kuwa kamouni tuliyoingi anayo mkataba ya GAS Entec imeuza share zake bila Serikali kuarifiwa. Waliouziwa, walipokuja walishangaa kuona ujenzi wa meli kwa sababu suala la ujenzi liko nje ya mauziano yao.”

Amesema ameshawasiliana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ambaye ameridhia hatua hiyo. “Ninamshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kuridhia hatua hii.”

Muonekano wa Meli ya MV Mwanza ‘Hapa Kazi Tu’

“Hawa watu wasiondoke hadi kazi ikamilike na kama wataondoka basi atakayewadhamini ni Balozi wao. Serikali tutaendelea kuwasiliana na Balozi wa Korea Kusini na tunaamini kazi hii itakamilika.”

“Haiwezekani tuwalipe hela hiyo, kazi haiendi kama ilivyopaswa. Tena wamepunguza Wafanyakazi kutoka 118 hadi 22, tunajuaje kama kesho watawaondoa hao 22 na wao wenyewe wapande ndege kurudi kwao, au waende Nairobi kupanda ndege.”

Mbali ya hilo, kampuni hiyo pia inadaiwa kupunguza wafanyakazi kutoka 118 hadi kufikia 22 hali inayosababisha ujenzi huo kusuasua licha ya serikali kulipa fedha za ujenzi huo kwa asilimia 80.

Ujenzi wa meli hiyo unatarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 97.5.

Ripoti ya CAG yampeleka Majaliwa Sengerema; Watumishi 30 mikononi mwa TAKUKURU
Majaliwa atua Mwanza kukagua miradi ya Maendeleo