Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kutoamini mitandao ya kijamii ambayo baadhi ya watumiaji wake huchapisha taarifa za uongo.

Waziri Mkuu ametoa rai hiyo mkoani Njombe mara baada ya kushiriki swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Wilaya ya Njombe ambapo amewataka Watanzania kuwa watulivu kwa kuwa Rais Dkt. John Magufuli yupo salama na anaendelea na majukumu yake.

Waziri Mkuu amesema, “Katika hili nataka kuonesha masikitiko yangu kwa baadhi ya watanzania ambao hawapendi maendeleo ya taifa letu wamejaa na chuki tu, wako nje ya nchi na wanatamani kuwachonganisha watanzania,”

“Tangu juzi mpaka leo asubuhi tunaona watanzania wenzetu wenye husda wanashawishi vyombo vya kimataifa wasema rais wa Tanzania anaumwa, kajifungia, tena hata hawapo Tanzania wapo nje. Sisi tupo ndani lakini tupo kimya. Wanaona fahari kuisema nchi yao vibaya,” amesema Majaliwa.

Waziri Mkuu amewataka Watanzania kuendelea kuliombea Taifa, huku viongozi wakitakiwa kukemea roho za chuki na kuhimiza kupendana.

Namungo FC kuivutia kasi Pyramid FC
Mukoko amlilia Kaze, awapa kazi wachezaji